Friday, August 28, 2009

‘FLASHBACK’ KATIKA FILAMU

Dhumuni la flashback katika filamu ni kumpa mtazamaji maelezo yanayohitajika katika kuifanya hadithi iendelee vizuri ama kutoa ufafanuzi wa matendo yanayofanywa na mhusika katika filamu.
Flashback inatakiwa kutumiwa pale tu kwenye ulazima wa kufanya hivyo, inatakiwa iwe ya tukio la kipekee ambalo linasherehesha kitendo anachokifanya mhusika kwa wakati huo.
Tukio hilo unaloliweka katika flashback lazima limfanye mtazamaji aelewe kuwa ndilo linalomsukuma mhusika atende kitendo akitendacho kwa muda huu.

HAPO VIPI?


MADIKODIKO!

Hii ni katika filamu ya 'MBWEMBWE'

WEWEEEEEEEE!

Usipimie hicho kichapo kwa staili hii hapa!

Saturday, August 8, 2009

JIELIMISHE!

Japo wanadai kuwa mada za mapenzi zinauza lakini naamini kuwa wanachoandika wasanii ama kuongelea ndio mwisho wa upeo wao wa uelewa.
Badala ya kutoa ujumbe watu wanashindana kuwaacha uchi waigizaji wa kike huku wenyewe wakishindana katika kuazima mavazi na magari ya kifahari.
Dhana hiyo ndiyo iliyopelekea baadhi ya wadau wa filamu kuwaambia wasanii wa kike wasiokuwa maarufu kwa kukaa uchi kuwa hawana mvuto! Ujinga huu.
Wanashindwa kuelewa kuwa wateja wao wakubwa ni kina mama na watoto, sasa unapomuonyesha mama yako au mdogo wako kichupi cha muigizaji wako wa kike ndio ubunifu?
Ili uweze kuelimisha jamii ni lazima kwanza ujielimishe mwenyewe!

Dah!

Mzee Magali katika A Girl from Nigeria!

Monday, August 3, 2009

UNALIA NJAA!!!!

Kuna wastani wa filamu tano ambazo huingizwa sokoni kila mwezi, haya ni makadirio yanayotokana na filamu ambazo hutangazwa sana na vyombo vya habari.
Lakini katika uhalisia, ni kwamba kuna kati ya filamu saba hadi kumi zinazoingizwa sokoni kila mwezi.
Katika mkutano mmoja wa wadau wa filamu uliofanyika hivi karibuni kuna mdau alitoa tathmini kuwa kuna zaidi ya maktaba laki moja zinazowakodisha filamu wananchi, na zote hizo zina wastani wa nakala halisi tatu tatu. Hizo ni mbali ya zinazonunuliwa kwa ajili ya kuangaliwa majumbani.
Tanzania ina watu takribani milioni arobaini, chukulia kuwa wateja wa filamu ni asilimia tano tu, basi hapo zitahitajika nakala milioni mbili.
Ukiongea na wasambazaji watakwambia kuwa filamu yenye mafanikio kuliko zote haijafikia nakala elfu hamsini! Ila kawaida nakala zinazotolewa hazifiki elfu kumi. Hazitoshi hata kusambazwa kwenye maktaba!
Hebu fikiria sasa, endapo filamu zinatoka nakala japo hizo laki tatu tu za kutosha maktaba, na bei ya nakala moja iwe ni shilingi elfu tatu.
Faida ikiwa mia tano tu, kila muvi mdau unapata milioni 150! Njaa itakuwepo?

FULL KUUZA!


Dennis 'akiuza nyago' filamuni

WA UKWELI?

Binti Sepetu, ni mkali ile mbaya filamuni na umissini. Kwingine? Sijui!

INAKUWAJE PALE?


Hapa wanaume kazini!

SWAHIBAAA!

Hapa ndio Richie anaingia na mzigo wake, Rose Ndauka huku 'Simba' JB akipata Kiroba. YAAN FULL MZUKA!

Hili ni pozi tu la 'kuuzia nyago'

Hapa 'Simba' JB naye analilipa pozi la Richie
Hawa jamaa USIWAPIMIE


WARSHA YA FILAMU MORO

Kundi la Mtazamo African Theatre limeandaa warsha ya uandishi na uandaaji wa filamu itakayofanyika katika hoteli ya MASUKA Village, Morogoro mwisho wa mwezi huu.
Warsha hiyo itaendeshwa na wataalamu toka Daraja Project, mradi wa filamu ulio chini ya taasisi ya Movie n' Style Tanzania.

BINTI KIZIWI AWA MISS KOROSHO TZ

Hii ni habari toka Morogoro ambapo Caroline ambaye ni kiziwi ameibuka kuwa Miss Korosho Tz baada ya kuwafunika mbaya vidosho wengine 11 Jumamosi 1/8/09 katika NANENANE Fashion week!

Saturday, August 1, 2009

HAPO VIPI?

Haji Adam akiwa na kimwana katika muvi inayokwenda kwa jina la Quick Money
Hapa Richa Adhia akiwa na kidume katika muvi inayoitwa Full Moon