Wednesday, July 22, 2009

Filamu MORO wamegoma!

Wadau wa filamu wa Morogoro hasa wasanii, wamegoma kuendelea kutumika na watengeneza filamu wa kutoka Dar kwa kucheza vipande vichache tu, sasa na wao wanataka kutengeneza za kwao ili wa Dar nao wacheze vipande vichache.

Jamal kutoka kundi la MTAZAMO la hapa mji kasoro bahari yuko Dar akifanya maongezi na taasisi ya Movie n' Style Tanzania (MSTZ) kuangalia uwezekano wa kuanza kuangusha maMuvi toka milima ya Uluguru!
KAENI CHONJO

MISS KOROSHO TANZANIA

Khabar ndo hiyo yakhe!
Kama unadhani umeshasikia kuhusu mashindano yote ya U-miss hapa Bongo, utakuwa umechemka.
Huku Morogoro kuna dude linadondoshwa linaitwa...
MISS KOROSHO TANZANIA
Ukitaka kujua vigezo na nani atatangazwa basi fika Hotel Oasis siku ya tarehe 1/8/2009.

Tuesday, July 21, 2009

KIPROFESHENO ZAIDI!

DARAJA PROJECT
We bring in Professionalism in filmmaking Tanzania
Wanaprofenisha muvi za kibongo, wanatoa huduma kwa gharama zinazoendana na hali halisi ya soko la Tanzania.
Scriptwriting, Directing, Production Management & Production Crew.
Wako 5th Floor MAVUNO HOUSE, Azikiwe Street, Dar es Salaam. Simu: o22 2125544 au 0784 235444

Mitindo Uluguruni!

Bonge la shoo la mitindo linatarajiwa kudondoshwa tarehe 1/8/2009 katika ukumbi wa Hotel Oasis, Morogoro kuanzia saa 2 usiku. Shoo hilo limepewa jina la.....

NANE NANE FASHION WEEK

Na linadondoshwa Mji Kasoro Bahari na Nepa Promotion chini Alex Nikitas. Itakuwa nomaaa!

Monday, July 20, 2009

Wa Filamu mpo?

Katika hotuba nzima iliyotolewa bungeni na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, kinachohusu filamu ni hiki:

Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza
66. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2009/10 Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza itatekeleza yafuatayo:
  • Kukagua na kupanga katika madaraja filamu 500 (Video, DVD, VCD na VHS) na kutoa vibali.
  • Kuandaa na kukamilisha mchakato wa kuandika kanuni za utekelezaji wa sheria Na. 4 ya mwaka 1976 ili zitangazwe na kusambazwa.
  • Kukusanya taarifa na takwimu za kumbi za sinema na michezo ya kuigiza ili kuzipanga katika madaraja. Kupitia na kuhakiki miswada ya utengenezaji wa filamu na kutoa vibali.
  • Kuhamasisha jamii na kutoa elimu kwa wadau 250 kuhusu kulinda, kuendeleza utamaduni, maadili na ujumi wa watanzania katika filamu na michezo ya kuigiza.

Mfuko wa Utamaduni (69 kipengele cha nne).

  • Kuwajengea uwezo na kuweka tarifa (capacity building and mapping) za watengeneza filamu wanaoinukia.

MNATEGEMEA NINI?

Saturday, July 18, 2009

Eti huyu kawa Afande..

Katika msako wa kumtafuta KUVETA, huyu jamaa alikuwa front kama Ditektive Lawrence. Hilo ni muvi moja hivi la 5 Effect ambalo wamekamua mastaa kibao, Big, Baba Haji, Mashaka, Bi Hindu, Kingwendu, Mkwere, Mzee Korongo, Mzee Msisi wa Msisiri na wengine kibao tu. SIJUI WATALIITAJE MUVI HILO kwa kuwa jina lake la awali (jina kapuni) kuna watu washaliigizia.

LINI TENA?

Mh. Bendera, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo akitoa Tuzo ya filamu bora kwa mwaka 2008.
Mzee Bawji, Wakurugenzi Octa na Galus wakiwa na Richard wa BBA II na Kanumba 'the Great'


Anko Richie wa UDSM akimtuza Emanuel (Kulia) huku Kanumba akishuhudia


Regina Dundelova (Kulia) wa EU Film Festival 08 akiwa kwenye Vinara 08


Jaji Cuthbert Kabunga (Kushoto) toka CMK Production akimkabidhi Tuzo Mpiga Picha bora, Rashid Mrutu




CHINA au TANZANIA?


Geti la Uwanja wa Taifa la Tanzania lakini limejengwa katika muundo wa utamaduni wa China. Au hamuoni nyumba zao kwenye mamuvi???

WAANDIKA MISWADA


Waandika Miswada wakiwa na Christian Wagner, mkali wa muvi toka Ujerumani (katikati ya waliokaa) baada ya warsha ya siku kadhaa iliyoandaliwa sambamba na European Film Festival, 2008.

Mwangalie hivi hivi.......


Ukitaka kuliona balaa la huyu mnayemwita Cloud basi mtazame akiitwa Dickson kwenye Sanda Nyeusi. Amerudi juu ile mbaya.

SHULE MUHIMU


Anko Richie akiwapiga shule ya Mswada (Script) waandishi wa filamu za kibongo




Mzee Amri Bawji, Ndambwe, Daudi Kulaya na wadau wengine wa filamu wakipata shule ya script toka kwa Mwalimu Richard Ndunguru wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika warsha iliyoandaliwa na Dot 5 Entertainment, 2007

Big a.k.a KUVETA



Huyu jamaa, amefunika mbaya akiitwa Kuveta katika muvi flani hivi linaloletwa na 5 Effects

SIFA ZA KIJINGA......


Friday, July 17, 2009

KAMA NI KWELI, MSIBA UKO NJIANI

Natoka kuongea na Mdau mwenzangu wa filamu za kibongo, ananiambia kuwa hali ni mbaya katika hoteli moja hapa Dar ambayo hutumika mara nyingi kama kambi wakati wa kutengeneza filamu mbali mbali.

Anamenidokeza kuwa ngono zinaendeshwa hovyo kati ya wasanii wa filamu zetu ambao tunawaona kama kioo cha jamii, tena ngono zenyewe ni zembe!

Sihitaji kuwafanyia udaku, lakini kama ni kweli msiba mkubwa unakuja mbele yetu kwa jinsi wanavyodaiwa kuzungukiana wenyewe kwa wenyewe!


ENDEKEZENI ELIMU SIO NGONO!

N'tamwambiaje?

Msomaji wangu mmoja wa makala ya Fumbua Macho inayotoka katika gazeti la Kiu ya Jibu kila Jumatatu aliniambia kuwa yeye ni mwanamke mwenye umri wa miaka 30 lakini hajawahi kufika kilele wakati wa ngono hata mara moja. Akaniuliza afanyeje?
Wiki iliyofuata nilimpa sababu za ujumla za kutofikia kilele ila karibu zote ni za kisaikolojia. Nilizungumzia pia ulazima wa mwanamke kuandaliwa kabla ya kulifanya tendo la kujamiiana.
Sasa ameniibukia mwingine mwenye tatizo kama hilo. Lakini huyu anasema tatizo ni mumewe hamuandai kabla ya kumuingilia na sasa wana miaka 6 ya ndoa.
Ananiuliza, 'nitamwambiaje aniandae?' Naomba tuchangiane mawazo

Wednesday, July 15, 2009

Filamu ya Sanda Nyeusi


Iko tayari kwa ajili ya walaji. Ukiikosa utakuwa umefanya kosa kwa maana ni taaaam sana!

Friday, July 10, 2009

Shirikisho la Filamu Tz

Uanzishwaji wa Shirikisho la Filamu huenda ukageuka kuwa igizo kama wadau wa filamu wenyewe hawatajizatiti katika kulifanikisha hilo.
Nauhisi ukosefu wa nia thabiti ya uanzishwaji wa shirikisho hilo, labda kwa kutoona umuhimu wake ama kuna watu wanaonufaika na hali ilivyo kwa sasa.
Toka kampeni ya uanzishwaji wa shirikisho hilo uanzishwe 8/5/2009 kwa kuundwa kamati ambayo na mimi nimo, sijaona harufu yeyote ya dhamira madhubuti ya wadau.
Ila kwa kuwa mimi binafsi siamini katika kushindwa, Punda atakufa lakini mzigo utafika.

Fumbua Macho za KIU

Kuanzia sasa muendelezo wa majadiliano kuhusu makala za Fumbua Macho kutoka katika gazeti la Kiu ya Jibu yatakuwa yakipatikana humu mtandaoni.