Thursday, December 17, 2009
HAIFANANISHIKI!
Friday, November 20, 2009
Saturday, November 14, 2009
MKOREA wa Filamu Tz!
Huyu anaitwa Park Doeng I, raia wa Korea ambaye amejitolea kuwasaidia wadau wa filamu Tanzania ili zipatikane filamu zenye ubora na viwango vya kimataifa, na ameanza na kikundi cha Safari Arts cha NIT, Dar. Hapa anaonyesha udugu kwa kum'beba mtoto wa kiswahili, tena mgongoni. Umeiona saa ya huyo mtoto?
Monday, November 9, 2009
Mtanashati!
Anti Ezekiel
Thursday, October 22, 2009
Tuesday, October 20, 2009
Monday, October 12, 2009
Long time baba'ake
Kwa sasa Mtitu (aliyekaa), kafungua ofisi ya kufa mtu maeneo ya magomeni inayojishughulisha na utengenezaji na usambazaji wa filamu.
Bravo Brother!
Bravo Brother!
Friday, October 9, 2009
Ni utumwa wa akili?
Friday, October 2, 2009
Thursday, September 17, 2009
JULIUS KAMBARAGE NYERERE
Suala sio tu kumkumbuka mzee huyu, wote tunamkumbuka. Tunamkumbukaje? hilo ndilo haswa tunalotakiwa kujiuliza katika nafsi zetu.
Wengi wanajidai kumfuata ili tu wapate muonekano mzuri mbele ya jamii ya watanzania, lakini moyoni mna yenu machafu!
Kama kweli mnamkumbuka hebu testini kurudisha
AZIMIO LA ARUSHA!
Wednesday, September 16, 2009
Changamoto
Ni sawa kudai haki yako, lakini unajua namna na wapi pa kuidai? hapa ndipo suala la shule linapokuja. Wasanii tutafute elimu!
Harakati za kudai haki bila kutumia akili ni sawa na kutaka kuzuia maji kwa godoro.
Friday, September 4, 2009
Friday, August 28, 2009
‘FLASHBACK’ KATIKA FILAMU
Dhumuni la flashback katika filamu ni kumpa mtazamaji maelezo yanayohitajika katika kuifanya hadithi iendelee vizuri ama kutoa ufafanuzi wa matendo yanayofanywa na mhusika katika filamu.
Flashback inatakiwa kutumiwa pale tu kwenye ulazima wa kufanya hivyo, inatakiwa iwe ya tukio la kipekee ambalo linasherehesha kitendo anachokifanya mhusika kwa wakati huo.
Tukio hilo unaloliweka katika flashback lazima limfanye mtazamaji aelewe kuwa ndilo linalomsukuma mhusika atende kitendo akitendacho kwa muda huu.

Friday, August 21, 2009
Saturday, August 8, 2009
JIELIMISHE!
Japo wanadai kuwa mada za mapenzi zinauza lakini naamini kuwa wanachoandika wasanii ama kuongelea ndio mwisho wa upeo wao wa uelewa.
Badala ya kutoa ujumbe watu wanashindana kuwaacha uchi waigizaji wa kike huku wenyewe wakishindana katika kuazima mavazi na magari ya kifahari.
Dhana hiyo ndiyo iliyopelekea baadhi ya wadau wa filamu kuwaambia wasanii wa kike wasiokuwa maarufu kwa kukaa uchi kuwa hawana mvuto! Ujinga huu.
Wanashindwa kuelewa kuwa wateja wao wakubwa ni kina mama na watoto, sasa unapomuonyesha mama yako au mdogo wako kichupi cha muigizaji wako wa kike ndio ubunifu?
Ili uweze kuelimisha jamii ni lazima kwanza ujielimishe mwenyewe!

Monday, August 3, 2009
UNALIA NJAA!!!!
Kuna wastani wa filamu tano ambazo huingizwa sokoni kila mwezi, haya ni makadirio yanayotokana na filamu ambazo hutangazwa sana na vyombo vya habari.
Lakini katika uhalisia, ni kwamba kuna kati ya filamu saba hadi kumi zinazoingizwa sokoni kila mwezi.
Katika mkutano mmoja wa wadau wa filamu uliofanyika hivi karibuni kuna mdau alitoa tathmini kuwa kuna zaidi ya maktaba laki moja zinazowakodisha filamu wananchi, na zote hizo zina wastani wa nakala halisi tatu tatu. Hizo ni mbali ya zinazonunuliwa kwa ajili ya kuangaliwa majumbani.
Tanzania ina watu takribani milioni arobaini, chukulia kuwa wateja wa filamu ni asilimia tano tu, basi hapo zitahitajika nakala milioni mbili.
Ukiongea na wasambazaji watakwambia kuwa filamu yenye mafanikio kuliko zote haijafikia nakala elfu hamsini! Ila kawaida nakala zinazotolewa hazifiki elfu kumi. Hazitoshi hata kusambazwa kwenye maktaba!
Hebu fikiria sasa, endapo filamu zinatoka nakala japo hizo laki tatu tu za kutosha maktaba, na bei ya nakala moja iwe ni shilingi elfu tatu.
Faida ikiwa mia tano tu, kila muvi mdau unapata milioni 150! Njaa itakuwepo?

WARSHA YA FILAMU MORO
Kundi la Mtazamo African Theatre limeandaa warsha ya uandishi na uandaaji wa filamu itakayofanyika katika hoteli ya MASUKA Village, Morogoro mwisho wa mwezi huu.
Warsha hiyo itaendeshwa na wataalamu toka Daraja Project, mradi wa filamu ulio chini ya taasisi ya Movie n' Style Tanzania.
BINTI KIZIWI AWA MISS KOROSHO TZ
Hii ni habari toka Morogoro ambapo Caroline ambaye ni kiziwi ameibuka kuwa Miss Korosho Tz baada ya kuwafunika mbaya vidosho wengine 11 Jumamosi 1/8/09 katika NANENANE Fashion week!
Saturday, August 1, 2009
Friday, July 24, 2009
Wednesday, July 22, 2009
Filamu MORO wamegoma!
Wadau wa filamu wa Morogoro hasa wasanii, wamegoma kuendelea kutumika na watengeneza filamu wa kutoka Dar kwa kucheza vipande vichache tu, sasa na wao wanataka kutengeneza za kwao ili wa Dar nao wacheze vipande vichache.
Jamal kutoka kundi la MTAZAMO la hapa mji kasoro bahari yuko Dar akifanya maongezi na taasisi ya Movie n' Style Tanzania (MSTZ) kuangalia uwezekano wa kuanza kuangusha maMuvi toka milima ya Uluguru!
Jamal kutoka kundi la MTAZAMO la hapa mji kasoro bahari yuko Dar akifanya maongezi na taasisi ya Movie n' Style Tanzania (MSTZ) kuangalia uwezekano wa kuanza kuangusha maMuvi toka milima ya Uluguru!
KAENI CHONJO
MISS KOROSHO TANZANIA
Khabar ndo hiyo yakhe!
Kama unadhani umeshasikia kuhusu mashindano yote ya U-miss hapa Bongo, utakuwa umechemka.
Huku Morogoro kuna dude linadondoshwa linaitwa...
MISS KOROSHO TANZANIA
Ukitaka kujua vigezo na nani atatangazwa basi fika Hotel Oasis siku ya tarehe 1/8/2009.
Tuesday, July 21, 2009
KIPROFESHENO ZAIDI!
DARAJA PROJECT
We bring in Professionalism in filmmaking Tanzania
Wanaprofenisha muvi za kibongo, wanatoa huduma kwa gharama zinazoendana na hali halisi ya soko la Tanzania.
Scriptwriting, Directing, Production Management & Production Crew.
Wako 5th Floor MAVUNO HOUSE, Azikiwe Street, Dar es Salaam. Simu: o22 2125544 au 0784 235444
Mitindo Uluguruni!
Bonge la shoo la mitindo linatarajiwa kudondoshwa tarehe 1/8/2009 katika ukumbi wa Hotel Oasis, Morogoro kuanzia saa 2 usiku. Shoo hilo limepewa jina la.....
Na linadondoshwa Mji Kasoro Bahari na Nepa Promotion chini Alex Nikitas. Itakuwa nomaaa!
NANE NANE FASHION WEEK
Na linadondoshwa Mji Kasoro Bahari na Nepa Promotion chini Alex Nikitas. Itakuwa nomaaa!
Monday, July 20, 2009
Wa Filamu mpo?
Katika hotuba nzima iliyotolewa bungeni na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, kinachohusu filamu ni hiki:
Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza
66. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2009/10 Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza itatekeleza yafuatayo:
Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza
66. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2009/10 Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza itatekeleza yafuatayo:
- Kukagua na kupanga katika madaraja filamu 500 (Video, DVD, VCD na VHS) na kutoa vibali.
- Kuandaa na kukamilisha mchakato wa kuandika kanuni za utekelezaji wa sheria Na. 4 ya mwaka 1976 ili zitangazwe na kusambazwa.
- Kukusanya taarifa na takwimu za kumbi za sinema na michezo ya kuigiza ili kuzipanga katika madaraja. Kupitia na kuhakiki miswada ya utengenezaji wa filamu na kutoa vibali.
- Kuhamasisha jamii na kutoa elimu kwa wadau 250 kuhusu kulinda, kuendeleza utamaduni, maadili na ujumi wa watanzania katika filamu na michezo ya kuigiza.
Mfuko wa Utamaduni (69 kipengele cha nne).
- Kuwajengea uwezo na kuweka tarifa (capacity building and mapping) za watengeneza filamu wanaoinukia.
MNATEGEMEA NINI?
Saturday, July 18, 2009
Eti huyu kawa Afande..
Katika msako wa kumtafuta KUVETA, huyu jamaa alikuwa front kama Ditektive Lawrence. Hilo ni muvi moja hivi la 5 Effect ambalo wamekamua mastaa kibao, Big, Baba Haji, Mashaka, Bi Hindu, Kingwendu, Mkwere, Mzee Korongo, Mzee Msisi wa Msisiri na wengine kibao tu. SIJUI WATALIITAJE MUVI HILO kwa kuwa jina lake la awali (jina kapuni) kuna watu washaliigizia.
LINI TENA?
Subscribe to:
Posts (Atom)