Kuna wastani wa filamu tano ambazo huingizwa sokoni kila mwezi, haya ni makadirio yanayotokana na filamu ambazo hutangazwa sana na vyombo vya habari.
Lakini katika uhalisia, ni kwamba kuna kati ya filamu saba hadi kumi zinazoingizwa sokoni kila mwezi.
Katika mkutano mmoja wa wadau wa filamu uliofanyika hivi karibuni kuna mdau alitoa tathmini kuwa kuna zaidi ya maktaba laki moja zinazowakodisha filamu wananchi, na zote hizo zina wastani wa nakala halisi tatu tatu. Hizo ni mbali ya zinazonunuliwa kwa ajili ya kuangaliwa majumbani.
Tanzania ina watu takribani milioni arobaini, chukulia kuwa wateja wa filamu ni asilimia tano tu, basi hapo zitahitajika nakala milioni mbili.
Ukiongea na wasambazaji watakwambia kuwa filamu yenye mafanikio kuliko zote haijafikia nakala elfu hamsini! Ila kawaida nakala zinazotolewa hazifiki elfu kumi. Hazitoshi hata kusambazwa kwenye maktaba!
Hebu fikiria sasa, endapo filamu zinatoka nakala japo hizo laki tatu tu za kutosha maktaba, na bei ya nakala moja iwe ni shilingi elfu tatu.
Faida ikiwa mia tano tu, kila muvi mdau unapata milioni 150! Njaa itakuwepo?

No comments:
Post a Comment