Friday, August 28, 2009

‘FLASHBACK’ KATIKA FILAMU

Dhumuni la flashback katika filamu ni kumpa mtazamaji maelezo yanayohitajika katika kuifanya hadithi iendelee vizuri ama kutoa ufafanuzi wa matendo yanayofanywa na mhusika katika filamu.
Flashback inatakiwa kutumiwa pale tu kwenye ulazima wa kufanya hivyo, inatakiwa iwe ya tukio la kipekee ambalo linasherehesha kitendo anachokifanya mhusika kwa wakati huo.
Tukio hilo unaloliweka katika flashback lazima limfanye mtazamaji aelewe kuwa ndilo linalomsukuma mhusika atende kitendo akitendacho kwa muda huu.

No comments:

Post a Comment