Saturday, July 18, 2009

CHINA au TANZANIA?


Geti la Uwanja wa Taifa la Tanzania lakini limejengwa katika muundo wa utamaduni wa China. Au hamuoni nyumba zao kwenye mamuvi???

WAANDIKA MISWADA


Waandika Miswada wakiwa na Christian Wagner, mkali wa muvi toka Ujerumani (katikati ya waliokaa) baada ya warsha ya siku kadhaa iliyoandaliwa sambamba na European Film Festival, 2008.

Mwangalie hivi hivi.......


Ukitaka kuliona balaa la huyu mnayemwita Cloud basi mtazame akiitwa Dickson kwenye Sanda Nyeusi. Amerudi juu ile mbaya.

SHULE MUHIMU


Anko Richie akiwapiga shule ya Mswada (Script) waandishi wa filamu za kibongo




Mzee Amri Bawji, Ndambwe, Daudi Kulaya na wadau wengine wa filamu wakipata shule ya script toka kwa Mwalimu Richard Ndunguru wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika warsha iliyoandaliwa na Dot 5 Entertainment, 2007

Big a.k.a KUVETA



Huyu jamaa, amefunika mbaya akiitwa Kuveta katika muvi flani hivi linaloletwa na 5 Effects

SIFA ZA KIJINGA......


Friday, July 17, 2009

KAMA NI KWELI, MSIBA UKO NJIANI

Natoka kuongea na Mdau mwenzangu wa filamu za kibongo, ananiambia kuwa hali ni mbaya katika hoteli moja hapa Dar ambayo hutumika mara nyingi kama kambi wakati wa kutengeneza filamu mbali mbali.

Anamenidokeza kuwa ngono zinaendeshwa hovyo kati ya wasanii wa filamu zetu ambao tunawaona kama kioo cha jamii, tena ngono zenyewe ni zembe!

Sihitaji kuwafanyia udaku, lakini kama ni kweli msiba mkubwa unakuja mbele yetu kwa jinsi wanavyodaiwa kuzungukiana wenyewe kwa wenyewe!


ENDEKEZENI ELIMU SIO NGONO!