Sunday, April 8, 2012

JIKUBALI!!!

USHAURI WA BURE! Ni vizuri ukiwa wewe na kuishi maisha yako kwa maana hakuna kama wewe katika dunia hii, ukijaribu kumuiga anayeishi maisha yake hakika maisha yatakushinda. Mwishowe utaombewa sana halafu utazidi kufua kwa kuwa hata Mungu ataona unamkera! Ignas

Monday, November 21, 2011

MOROGORO

Wenyeji wanauita ni mji kasoro bahari, lakini wangeuita Mji wenye milima na Dar ndio lingekuwa jiji kasoro milima. Waonaje?

Friday, March 12, 2010

Tuesday, January 19, 2010

'GAME OVER'

Tamaa inapopelekea mtu kumsaliti rafiki yake, lakini daima msaliti hashindi! Usikose kuiona filamu hii, 'Game Over'!

Tuesday, January 12, 2010

ASALI CHACHU!

Filamu ya Asali Chachu iko tayari na muda wowote itakuwa sokoni.

Thursday, December 17, 2009

HUYU NDIYO NYOTA!

JAMILA (Latifa Idabu)
Aling'ara kwenye filamu ya Sanda Nyeusi


Kafunika kwenye ASALI CHACHU


Cheki hili pozi, hafi mtu kweli hapa?!



HAIFANANISHIKI!

ASALI CHACHU!
ASALI CHACHU ni filamu ambayo huwezi kuifananisha na yeyote kati ya ambazo umewahi kuziona katika maisha ya filamu za kibongo.
ASALI CHACHU ni filamu daraja kati ya filamu za burudani na filamu za kuelimisha, unaelimuka huku ukiburudika.

ASALI CHACHU ni filamu ambayo unaweza kuiangalia na familia yako, haijatengenezwa na wale wanaoamini kuwa kuacha vichupi nje ndiyo filamu inauza.